KANDA YA ZIWA KUWA NA VITUO VIWLI HUDUMA BOBEZI YA MOYO

 

KANDA YA ZIWA KUWA NA VITUO VIWLI  HUDUMA BOBEZI YA MOYO

KANDA YA ZIWA KUWA NA VITUO VIWLI  HUDUMA BOBEZI YA MOYO

GEITA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kuifanya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato kuwa kituo cha umahiri wa matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi wa moyo ili kuipa nguvu hospitali ya kanda ya Bugando.
Kanda ya Ziwa ina watu takribani milioni 22, hivyo serikali imeona ipo  haja ya kuwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda nyingine katika ukanda wa ziwa(Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Kagera pamoja na Kigoma na ianze kutoa huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi wa moyo katika ukanda huo wa ziwa.
Kwa hatua hii, huduma  za magonjwa ya moyo za watu wa Kanda ya ziwa  zitaishia Chato ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo karibu na wananchi  pamoja na kupunguza msongamano wa wagonjwa wa moyo JKCI – Dar es Salaam.