GEITA NA BARABARA ZA NJIA NNE

GEITA NA BARABARA ZA NJIA NNE

 GEITA NA BARABARA ZA NJIA NNE

GEITA
Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Barabara (Tanroads) imetangaza kuja na mpango wa upanuzi wa mtandao wa barabara kuu mjini Geita kwa mfumo wa njia nne umbali wa Km 24 ili kupunguza msongamano.
Upanuzi huo wa barabara unaenda sambamba na ujenzi wa njia mchepuko (By pass) ili kupunguza adha ya magari makubwa kupita katikati ya mji wa Geita iwapo hakuna ulazima.
Mradi huo wa upanuzi wa barabara kwa njia nne kwa sasa upo kwenye hatua ya upembuzi yakinifu na mara baaada ya kukamilika tenda itatangazwa na gharama ya mradi itafahamika.
Aidha Mji wa Geita unakua kwa kasi sana, kwani kwa uchimbaji na biashara ya dhahabu, Geita ndio inaongoza, kwa hiyo mji huo unakabiliwa na ongezeko kubwa la magari
KWA TAARIFA YAKO:- mpaka sasa mkoa wa Geita una mtandao wa barabara wa Km 1019.13 katika mtandao huo kuna km 236 ambazo ni barabara kuu na zilizobaki ni barabara za mkoa, Pia Katika mtandao wote wa barabara kuna kilomita 401 ambazo ni barabara za lami kwa mkoa mzima kwa kujumuisha madaraja na makalavati 305.