GEITA KUCHORONGOA MADINI KISASA

 

GEITA KUCHORONGOA MADINI KISASA

GEITA KUCHORONGOA MADINI KISASA

GEITA
Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limekabidhi mtambo wa uchorongaji kwa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo mkoani Geita (Gerema) ambao umeanza kazi kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za kijiolojia.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika mgodi wa mfano uliopo kata ya Lwamugasa wilayani Geita mkoani hapa lengo likiwa ni kuwasaidia wachimbaji wadogo waachane na uchimbaji wa kubahatisha.
Kutolewa kwa mtambo wa  uchorongaji  Geita utaondoa tatizo la kuchimba bila taarifa sahihi za kijiolojia, hali ambayo ilikuwa inapelekea kupoteza mtaji , kutokuaminika na taasisi za kifedha na matumizi ya imani potofu.
Aidha mtambo huo ni miongoni mwa mitambo mitano iliyonunuliwa na serikali kupitia  Stamico ambapo tayari imefanyiwa majaribio na kuonyesha matokeo chanya katika migodi ya Nyamongo mkoani Mara, Chunya mkoani Mbeya na migodi iliyopo Dodoma mitambo hiyo imechoronga vizuri na mwitikio wa wachimbaji wadogo ni mkubwa.
Shirika la madini la Taifa limejipanga ifikapo Aprili 2024 tayari itaingia mitambo mingine mitano na ifikapo mwisho wa mwaka huu wa fedha ambao ni Juni itakuja tena mingine mitano jumla itakuwa 15.