DKT SAMIA KUONGOZA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

 

DKT SAMIA KUONGOZA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

DKT SAMIA KUONGOZA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA 

Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan (leo)  Machi 4 ataongoza  ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola (CLMM) unaofanyika kila baada ya miaka miwili kuanzia leo hadi Ijumaa wiki hii.
Maandalizi ya hafla hiyo kubwa yamekamilika na wajumbe walianza kuwasili nchini kuanzia mwishoni mwa wiki, kwa mujibu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola.
Aidha Wakati wa mkutano mawaziri wa sheria na wanasheria wakuu kutoka katika nchi 56 za Jumuiya ya Madola watajadili maendeleo ya hivi majuzi ya kisheria katika mamlaka zao ikiwa ni pamoja na mali za kidijitali, rasilimali za kielektroniki kwa mifumo bora ya sheria, ulinzi wa wanawake na wasichana, kuimarisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu na maendeleo ya sera na sheria za hali ya hewa
Lengo kuu litakuwa katika kuchunguza njia zinazowajibika za kutumia teknolojia ili kuboresha sheria na upatikanaji wa haki, hasa kwa watu waliotengwa.
FAIDA YA KUFANYIKA MKUTANO HUU NCHINI
Upatikanaji wa fursa nzuri kwa Watanzania kuhusu masuala ya uchumi, maendeleo ya kijamii na kisiasa.