BUGANDO KUANZA UPANDIKIZAJI FIGO
MWANZA
Serikali kupitia Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, mkoani Mwanza itaanza kutoa huduma za upandikizaji figo mwishoni mwa mwaka huu.
Hatua hiyo ni kufuatia ongezeko la wagonjwa wa figo, ambapo hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wapya kati ya 15 hadi 20 kwa siku, kutoka wanne kwa siku wakati Bugando inaanzisha matibabu ya figo, miaka ya 1970.
Hatua hii inakuja baada ya serikali ya awamu ya sita kuendelea kufanya maboresho sekta ya afya kwa kuongeza mashine za kusafishia figo takribani 27 na sasa inaelekea kuwezesha utoaji huduma ya uhakika kwa kupandikiza figo, ambayo itamuwezesha mgonjwa kurudi hali yake ya zamani.
