“4R ZINANISAIDIA KUONGOZA TAIFA”DKT SAMIA

 

“4R ZINANISAIDIA KUONGOZA TAIFA”DKT SAMIA

“4R ZINANISAIDIA KUONGOZA TAIFA”DKT SAMIA

DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  Samia Suluhu Hassan amesema njia shirikishi ya kuliongoza Taifa imekuwa mbinu muhimu na mkakati maalum katika uongozi wake hasa kupitia  falsafa za 4R ((Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding) 
Mhe Rais Samia ameyasema hayo (jana) alipokuwa akizungumza kwenye The Citizen Rising Woman hafla iliyoandaliwa na Mwananchi Communications Ltd (MCL) iliyofanyika ukumbi wa The Super Dome Masaki wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Dar es Salaam, 08 Machi, 2024.
“Nashukuru kwamba falsafa ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding) imepokelewa vyema na Watanzania. Falsafa hiyo inanisaidia kushirikisha watu wengi katika kufanya maamuzi, ikiwa ni pamoja na kupanga njia ya kusonga mbele ninapoongoza taifa” Amesema Mhe Rais Samia.
Dkt Samia ameongeza “Naamini maamuzi ya kuendesha nchi yanabaki kuwa jukumu la kila Mtanzania, ushirikishaji ni njia niliyoichagua katika kuendesha nchi.”
Katika hatua nyingine, Mhe Rais amesisitiza malezi bora ili kuwawezesha watoto kuwa raia wa kuwajibika, akisema binadamu yeyote aliyeumbwa na Mungu ana uwezo wa kufanya jambo jema kwa jamii.
"Tukiwalea watoto wetu katika maadili mema watafanya maajabu," ameeleza.