UJENZI WA VIVUKO VITANO WAFIKIA 80%

 

UJENZI WA VIVUKO VITANO  WAFIKIA 80%

UJENZI WA VIVUKO VITANO  WAFIKIA 80%

MWANZA 
Ujenzi wa vivuko vitano vinavyotarajiwa kutumika katika wilaya za Ukerewe, Sengerema, Magu na Bunda umefikia asilimia 80  huku Kampuni ya Songoro Marine ikiendelea na ujenzi wa vivuko vipya kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo ya Buyagu na Mbalika Wilayani Sengerema, Ijinga na Kahangala Wilayani Magu, Bwiro na Bukondo Wilayani Ukerewe, Nyakaliro na Kome Wilayani Sengerema pamoja na Kisorya Wilayani Bunda Mkoani Mara na Rugezi Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.