TSH TRILIONI 2.5 KUBORESHA RELI YA TAZARA
ZAMBIA
Jumla ya Shilingi trilioni 2.5 ( Dola 1 bilioni za Marekani)zinatarajiwa kutumika kwa ajili
ya matengenezo ya reli ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara), yenye umri wa karibu miongo mitano sasa.
Taarifa kuhusu gharama za maboresho ya reli hiyo, imetolewa na Balozi wa China nchini Zambia, Du Xiaohui, hivi karibuni.
Reli hiyo inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Mji wa Kapiri Mposhi nchini Zambia ni miongoni mwa miradi ambayo China ilifadhili ujenzi wake uliokamilika mwaka 1975.Mapema wiki iliyopita, Xiaohui aliwasilisha pendekezo la mradi wa matengenezo ya reli hiyo kwa Waziri wa Usafirishaji wa Zambia, Frank Tayali.