TSH MIL 475+ ZAJENGA SHULE MPYA YA MSINGI YA IGIMA (MLIMBA)

 

TSH MIL 475+ ZAJENGA SHULE MPYA YA MSINGI YA IGIMA (MLIMBA)

TSH MIL 475+ ZAJENGA SHULE MPYA YA MSINGI YA IGIMA (MLIMBA)

MOROGORO

Serikali imepeleka kiasi cha shilingi milioni 475.3  kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa shule ya Msingi Igima ikiwa ni mpango wa utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) katika Wilaya ya Mlimba mkoani Morogoro.

Shule hiyo mpya hadi sasa imekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 16, vyumba 2 vya madarasa ya awali, jengo la utawala, matundu ya vyoo 28.

Kukamilika kwa mradi huo kumekuwa na faida ya kuondokana na msongamano wa wanafunzi darasani, kusogeza huduma ya shule karibu katika jamii na kuongeza kiwango cha uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule.