TSH BIL 449.92 ZANUNUA PEMBEJEO 2022/2023
DAR ES SALAAM
Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha kuwa wakulima na wanachama wa Vyama vya Ushirika wanahudumiwa kwa kusogezewa huduma karibu, imesogeza jukumu kwa Vyama vya ushirika kuratibu upatikanaji pamoja na usambazaji wa pembejeo za kilimo nchini.
Hadi kufikia tarehe 30 Machi, 2023, jumla ya shilingi 449,922,623,196 zilitumika kunununua pembejeo za kilimo kupitia Vyama vya Ushirika kwa ajili ya wakulima wa mazao mbalimbali.
Aidha Mbolea iliyonunuliwa na kusambazwa kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika ni Tani 1,266,435 yenye thamani ya Shillingi bilioni 227.98.