SULUHU YA UMEME MIGODINI KUPATIKANA

 

SULUHU YA UMEME MIGODINI KUPATIKANA

SULUHU YA UMEME MIGODINI KUPATIKANA

DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanza mazungumzo na Kampuni ya TAQWA-DALBIT kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa upatikanaji wa nishati ya umeme migodini na maeneo yenye wachimbaji wadogo ili kuchochea shughuli za uchimbaji madini nchini Tanzania.
Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dodoma yakiongozwa na na wizara ya madini pamoja na Menejimenti ya Uongozi wa Kampuni ya TAQA-DALBIT ikiongozwa na Meneja Mkuu Amr Aboushad na Mkurugenzi wa maendeleo ya Biashara Raphael Banzi.
Akiwasilisha maelezo ya awali, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Amr Aboushad amesema wapo  tayari kuzalisha umeme kupitia gesi kwa kufunga mtambo katika migodi na maeneo ya wachimbaji.
Amesema kufungwa kwa mitambo hiyo kutasaidia  kupunguza gharama za uzalishaji kwa zaidi ya nusu ya gharama inayotumika hivi sasa kupitia matumizi ya mafuta ya dizeli na petrol,pia kampuni itahusika na uzalishaji wa umeme kupitia mfumo wa umeme jua ambapo itafunga mtambo mkubwa kwa gharama yao na kuwaunganisha wachimbaji wadogo kwa malipo ya mwezi ya matumizi ya nishati hiyo.