TSH MIL 199 YABORESHA SHULE YA JANGWANI SEKONDARI
DAR ES SALAAM
Serikali ya Awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi Milioni 199 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 8 pamoja na matundu ya vyoo 13 katika shule ya Shule ya Sekondari ya Jangwani iliyopo Ilala Dar es salaam
Lengo la ukarabati/ujenzi ni kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu ili kuendana na dhana ya Dkt Samia ya kutoa elimu bure hivyo urahisishaji wa upatikanaji wa elimu, uendane na Mazingira ya kufundishia na kujifunzia.