TSH BIL 700 ZAJENGA GHALA ZA MAZAO NCHINI
DAR ES SALAAM
Katika kuendelea kuboresha wizara ya kilimo, serikali ya awamu ya sita kupitia wizara tajwa imetumia kiasi cha shilingi bilioni 700 kukamilisha ukarabati na ujenzi wa ghala na vihenge katika maeneo mbalimbali nchini.
Wizara kupitia CPB imekamilisha ukarabati wa ghala la Kiteto Mkoani Manyara (tani 1,000); Mbugani Mkoani Dodoma (tani 30,000) na vihenge Mkoani Arusha (tani 38,000).
Aidha, hadi Aprili, 2022 ukarabati wa ghala tisa (9) katika Halmashauri za Wilaya za Songea na Madaba umefikia hatua mbalimbali kama ifutavyo: Songea DC - Mkongotema (89.5), Muungano Zomba (64.74), Litisha (48.67), Magagura (55.09), Lipaya (21.58); Madaba DC - Hagangadinda (57.8), Matetereka (45.13) Lilondo B (83.5) na Gumbiro (96.28). Ukarabati huo unahusisha sakafu, kuta, paa, vyoo na kuweka mfumo wa maji.