NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA KUKUTANA ZANZIBAR
ZANZIBAR
Tanzania imepata heshima kubwa ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 8 Machi 2024, kwa takriban miaka10 iliyopita, sasa ni mara ya kwanza kufanyika mkutanohuo nchini ambao utahudhuriwa na wageni zaidi ya 300 kutoka nchi 56 wanachama wa Jumuiya ya Madola.
Sababu zilizopelekea Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni vigezo vya amani na utulivu ikiwa ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii katika pande mbili zote za Muungano wa Tanzania.
Aidha Tanzania inaendelea kuwa mfano wa utawala bora kupitia muhimili wa Mahakama hasa katika utawala wa sheria,kwa wananchi kupata huduma mbalimbali za kisheria hasa kwa watoto.