TANI 33 ZA SUKARI ZAWAPA AHUENI WAKAZI WA RUKWA
RUKWA
Wakazi wa Mkoa wa Rukwa wamepumua kufuatia kuwasili kwa shehena ya kwanza ya tani 33 za sukari ili kumudu mahitaji ya sasa na kushusha bei ya bidhaa hiyo inayozidi kupanda juu.
Upakuaji wa mizigo hiyo kwenye malori katika mji wa Sumbawanga ulifanyika kwa utulivu na kushuhudiwa na viongozi wa Wilaya ya Sumbawanga na mamia ya wananchi.
Katika mapokezi ya shehena hiyo, ofisi ya Mkuu wa wilaya Sumbawanga, imewaambia waandishi wa habari kuwa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) imeidhinisha kutenga tani 132 za sukari kwa Rukwa kutoka kwa wazalishaji wa sukari,ambapo
hadi sasa shehena ya kwanza ya tani 33 za sukari imewasili mjini Sumbawanga ambayo shehena iliyobaki ya tani 99 inatarajia kuwasili hivi karibuni.
Bei elekezi ya Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) imebaki kati ya shilingi 2,800/- hadi 3,200/- kwa kilo moja kulingana na eneo la Rukwa, Kigoma na Mkoa wa Katavi bei ya jumla ni kati ya 2,600 na 2,800/- wakati bei ya rejareja ni 3,200