TSH BIL 899 KULIPA POSHO WAHUDUMU WA AFYA

tsh bil 899 kulipa posho wahudumu wa afya

TSH BIL 899 KULIPA POSHO WAHUDUMU WA AFYA

DODOMA
Serikali inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 899 kufundisha na kuwalipa posho ya kila mwezi wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao laki 137,294 ili kutoa elimu ya afya, Lishe na kupinga ukatili wa kijinsia kwenye jamii. 
Wahudumu hawa watakuwa wawili kwa kila Mtaa (Mitaa yote 4,263) na wawili kwa kila kitongoji (Vitongoji 64,384) ili kutoa elimu ya afya, lishe na kupinga ukatili wa kijinsia.