HATI FUNGANI YA SAMIA YANUKIA KWA WAKANDARASI

 

hati fungani ya samia yanukia kwa wakandarasi

HATI FUNGANI YA SAMIA YANUKIA KWA WAKANDARASI

DAR ES SALAAM
Serikali kupitia  wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  imeielekeza Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na taasisi za fedha nchini kuanzisha mchakato wa upatikanaji wa hati fungani ya miundombinu ya barabara (Tarura Infrastructure Bond).
Lengo la hati funguani hiyo ambayo itapewa jina la ‘Samia Bond’ ni kuwawezesha Makandarasi wa ndani mitaji.
Chanzo:- Tamisemi kupitia kikao kazi na Menejimenti ya Tarura, Makatibu Tawala Wasaidizi Miundombinu, Makandarasi Wazawa, Wataalamu Washauri na Taasisi za Kibenki, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Hati fungani hii italeta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya miundombinu ya Barabara inayojengwa na TARURA na itaendana na kasi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwashirikisha na kufanya kazi na sekta binafsi, katika kutatua na kubuni mbinu za kuchochea gurudumu la kuwafikishia maendeleo wananchi