TSH BIL 837.8 ZIMETOLEWA KWA SERIKALI ZA MITAA

 

TSH BIL 837.8 ZIMETOLEWA KWA SERIKALI ZA MITAA

TSH BIL 837.8 ZIMETOLEWA KWA SERIKALI ZA MITAA

DODOMA
Serikali ya awamu ya sita imetoa kiasi cha  Sh Bilioni 837.8 kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zimetumika katika ujenzi wa shule za Sekondari mpya 486, vyumba vya madarasa 21,990, nyumba za walimu 280, mabweni 221, ukarabati wa shule kongwe 21, maabara 151 na mabwalo 23.
Utolewaji wa fedha hizo zimeboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia shuleni ambazo zimeongeza udahili wa wanafunzi wa elimu ya awali msingi na sekondari pamoja na kuimarika kwa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne.