TSH BIL 6.5 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO USHETU
SHINYANGA
Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga imepokea zaidi ya Sh bilioni 6.5 sawa na 55% ya bajeti iliyotengwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Kiasi hicho kimetumika katika utekelezaji wa miradi katika nusu mwaka kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba
Hadi sasa miradi yote imekamilika iliyokuwa kwenye mipango ambayo ni matundu 66 ya vyoo yaliyojengwa kwenye shule za msingi kumi ,ukamilishaji wa jengo la mama na mtoto kituo cha afya Igwamanoni na ujenzi wa sekondari moja kata ya Ulowa.
