ZIARA YA RAIS WA POLAND KUONGEZA UTALII, UWEKEZAJI NCHINI

 

ZIARA YA RAIS WA POLAND KUONGEZA UTALII, UWEKEZAJI NCHINI

ZIARA YA RAIS WA POLAND KUONGEZA UTALII, UWEKEZAJI NCHINI 

DAR ES SALAAM
Rais wa Poland Andrzej Duda ameeleza utayari wa nchi yake (Poland) kuimarisha ushirikiano na Tanzania, hususan katika maendeleo ya sekta ya utalii na kuongeza uwekezaji wa Poland nchini.
Rais Duda ameeleza dhamira hiyo katika hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam (Ijumaa) Februari 9 muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo baina ya nchi hizo mbili na Rais  wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kufuatiwa na mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.
“Ninayofuraha kutangaza kwamba Poland ina hamu ya kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika sekta mbalimbali, zikiwemo utalii na uwekezaji,” Rais Duda amesema.
Aidha ameongeza"Kundi kubwa la wajasiriamali wa Poland wameonesha nia ya kushirikiana katika ubia wa kisasa wa tasnia, kama vile miundombinu ya mijini, usimamizi wa rasilimali za maji, mifumo ya benki ya kidijitali, na vile vile teknolojia ya habari na mawasiliano”
 Hali kadhalika Rais Duda amekumbuka ukarimu uliotolewa kwa wakimbizi 7,000 wa Poland, ambao walitafuta hifadhi nchini Tanzania wakati wa Vita Kuu ya II, ambayo iliacha hisia ya kudumu ya shukrani ndani ya jumuiya ya Poland.
Mhe Rais Duda, pamoja na mwenzi wake Agata Kornhauser Duda, pamoja na ujumbe wa Poland  walianza ziara nchini Tanzania tarehe 8 hadi 9 Februari 2024.
KUMBUKA:- Ziara hiyo imelenga kuimarisha uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi kati ya Tanzania na  Poland