TSH BIL 8.4 KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI UJIJI

 

TSH BIL 8.4 KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI UJIJI

TSH BIL 8.4 KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI UJIJI

KIGOMA
Serikali imeidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 8.4 ili kutekeleza shughuli mbalimbali za kutoa na kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji na vitongoji vyake.
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha ni ukarabati wa miundombinu chakavu, kuongeza mtandao wa bomba za maji katika maeneo ya Kazegunga, Kagera, Mwasenga, Businde, Kasaka, Kalalangabo na Buronge.
KUMBUKA:- Serikali imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi ikiwemo huduma ya maji safi na salama