SWEDEN YAKABIDHI TSH BIL 210 ZA ELIMU

 

SWEDEN  YAKABIDHI TSH  BIL 210 ZA ELIMU

SWEDEN  YAKABIDHI TSH  BIL 210 ZA ELIMU

DAR ES SALAAM
SERIKALI imesaini makubaliano ya ruzuku ya dola milioni 84 sawa na shilingi bilioni 210 na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kusaidia walimu.
Chanzo:- Charlotta-Ozaki Macias, balozi mkazi wa Uswizi katika hafla ya utiaji saini Hazina jijini Dar es Sa-laam
Fedha hizo zimetolewa kwa ushirikiano na shirika la Global Partnership for Education (GPE) lenye makao yake makuu mjini Washington.
Mpango wa tatu wa miaka mitano kuanzia 2021/22 hadi 2025/26, unatafuta uchumi shindani na wa viwanda kwa maendeleo ya binadamu ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu au Dira ya 2030 ambapo kutoa ujuzi na kujifunza kwa kujitegemea,ajira ni muhimu