TSH BIL 1.9 KUKAMILISHA MIRADI 108 YA MAJI MISUNGWI MWANZA

TSH BIL 1.9 KUKAMILISHA MIRADI 108 YA MAJI MISUNGWI MWANZA

TSH BIL 1.9 KUKAMILISHA MIRADI 108 YA MAJI MISUNGWI MWANZA

Takribani miradi 108 ya jamii wilayani Misungwi mkoani Mwanza, yenye thamani zaidi ya Sh billioni 1.9 iko ukingoni kukamilika, huku wananchi wakiipongeza serikali kwa hatua hiyo.
Ni miradi inayotekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF), kama sehemu ya mpango wa kunusuru kaya maskini, awamu ya tatu ya kipindi cha pili, iliyoanza mwaka 2020 na itamalizika 2025.
Miradi nane ni ya mabwawa kwa ajili ya mifugo kunywa maji, maarufu kama ‘lambo’ na 100 ni ya barabara.