WAWEKEZAJI 901 WAWEKEZA NCHINI MWAKA 2024
TANZANIA
Kituo Cha Uwekezaji Nchini (TIC) kwa mwaka 2024 kimefanya usajili wa miradi ya wawekezaji 901 kutoka miradi 500 ya mwaka 2023 ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 44.5.
Miradi 500 ya uwekezaji iliyosajiliwa mwaka 2023 ina thamani ya dola za kimarekani bilioni tano (sawa na shilingi 1,253,750,000,000) huku miradi 901 iliyosajiliwa mwaka 2024ina thamani ya dola za kimarekani bilioni 9.3 ( shilingi 2,331,975,000,000)
Mafanikio hayo yametokana na uboreshaji wa mazingira bora ya uwekezaji pamoja na mabadiliko ya uwekezaji mwaka 2022 ambayo imeondoa vikwazo vingi kwenye usajili wa uwekezaji,pia kwa sasa TIC ina kituo cha One Stop Center ambapo usajili wa miradi huduma zote hupatikana sehemu moja na ukamilishaji unafanyika ndani ya siku tatu pekee.