DKT SAMIA KWENDA VATICAN FEBRUARI 11 NA 12 KWA MWALIKO WA PAPA FRANCIS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara katika Mji wa Vatican na kufanya mazungumzo na Papa Februari 11 na 12, 2024.
Ziara ya Dkt Samia mjini Vatican ni baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis.
Dkt Samia ataenda na Waumini kuanzia viongozi wa Jumuiya, Umoja wa Vijana Wakatoliki (VIWAWA), umoja wa Wanawake wakatoliki (WAWATA).
Aidha Rais Samia akiwa Vatican atakutana kwa mazungumzo na Baba Mtakatifu Francis pamoja na Katibu wa Vatican, Pietro Parolin.
#DIPLOMASIAINALIPA
