TSH BIL 3 ZAJENGA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA LONGIDO
ARUSHA
Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari iliyopewa jina la” Longido Samia Girl’s Sekondari” ya masomo ya Sayansi ambayo itaanza kutoa elimu mwezi huu wa Februari ili kuwezesha watoto jamii ya wafugaji kusoma na kupata wasomi wengi nchini wanaoweza kujiajiri wenyewe.
Samia Girls Sekondari imejengwa ikiwa na lengo la kuleta mapinduzi makubwa ya elimu kwa jamii hiyo.
