TSH BIL 208 KUJENGA SHULE MPYA ZA SEKONDARI
DAR ES SALAAM
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya sh. bilioni 208 ili zitumike kujenga shule mpya za sekondari kwenye Halmashauri zote 184 nchini.Kila Halmashauri imepatiwa kiasi cha shilingi milioni 570 hadi milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa shule hizo mpya za sekondari.
