PEMBEJEO ZA RUZUKU ZAWAINUA IRINGA

 

PEMBEJEO ZA RUZUKU ZAWAINUA IRINGA

PEMBEJEO ZA RUZUKU ZAWAINUA IRINGA

IRINGA
Mkoa wa Iringa umepata ongezeko kubwa la uzalishaji wa sekta ya kilimo hadi zaidi ya tani milioni moja mwaka 2023 kutoka tani 800,000 kabla ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kushika madaraka yake.
Kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao kunatokana na kilimo cha kisasa kwa kutumia mbolea na huduma za ugani zinazosimamiwa na serikali ya awamu ya sita kwa lengo la kuondokana na kilimo cha kujikimu na kuingia kibiashara.
Chanzo:- ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Mafanikio hayo yametokana na kuanzishwa kwa mbolea ya ruzuku ya serikali iliyotolewa kwa wakulima, huku matumizi ya mbolea mkoani Iringa yakiongezeka hadi tani 47,000 mwaka jana kutoka 19,000 mwaka uliopita.