TANZANIA NA KOREA KUSINI KUBORESHA JIJI LA DODOMA

 

TANZANIA NA KOREA KUSINI KUBORESHA JIJI LA DODOMA

TANZANIA NA KOREA KUSINI KUBORESHA JIJI LA DODOMA

DAR ES SALAAM
Ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Korea Kusini  umechochea kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ikiwemo mradi wa kimkakati wa daraja la Tanzanite lililojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini kupitia mfuko wa ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi (Economic Development Cooperation Fund -EDCF).
Chanzo:- Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na uratibu wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano yaliyohusisha Ofisi ya Waziri Mkuu na National Agency for Adminstrative City Constraction and Heerim Architects and Planners ya Nchini Korea Kusini
Kupitia kusainiwa kwa hati hizo Tanzania itanufaika na teknolojia ya kisasa ya usanifu na ujenzi wa majengo na miundombinu mingine itayopendezesha mji mkuu Dodoma, sambamba na kupatikana kwa fursa mpya za ushirikiano na makampuni ambayo yana uzoefu mkubwa wa usanifu na ujenzi hususani wa majengo katika miji na majiji makubwa.