DKT SAMIA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA NAMIBIA
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 7 Februari 2024 amesaini kitabu cha maombolezo
ya Rais wa Namibia Hayati Dkt. Hage G. Geingob Masaki Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kusaini kitabu cha maombolezo Mhe Rais Samia amefanya mazungumzo na Viongozi, Watumishi wa Ofisi ya Ubalozi huo wa Namibia.
Hayati Hage G. Geingob amefariki mapema Jumapili Februari 4, 2024 akiwa na umri wa miaka 82.
