TSH BIL 119+ KUBORESHA HUDUMA YA MAJI LINDI
LINDI
Serikali kupitia wizara ya maji inatekeleza ujenzi wa Mradi wa Maji wa vijiji 34 vya wilaya ya Ruangwa na Vijiji 21 vya Wilaya ya Nachingwea kutoka Chanzo cha mto Nyangao mkoani Lindi.
Mradi ulianza tarehe 18/02/2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 28/04/2025 ambapo unatarajiwa kuwanufaisha wananchi 128,657 wa Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea
