DKT SAMIA AKUTANA NA PAPA FRANCIS VATICAN

DKT SAMIA AKUTANA NA PAPA FRANCIS VATICAN

 DKT SAMIA AKUTANA NA PAPA FRANCIS VATICAN

VATICAN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan  amekutana na kufanya mazungumzo na Papa Francis katika Mji wa Vatican (jumatatu) tarehe 12 Februari 2024 ikiwa ni ziara yake ya siku mbili, hii ni baada ya  Dkt Samia kupokea mwaliko kutoka Kwa papa Francis.
Katika mazungumzo yao ya faragha wamejadili kuhusu kuhimiza amani duniani.
Baada ya kukutana na Papa Francis Mhe Rais Samia amekutana na katibu wa jimbo la Vatican Kardinali Pietro Parolin akifuatana na katibu wa Vatican anayeshughulikia Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Holy See Press Office inasema "majadiliano yalikuwa mazuri,ambayo yameangazia mahusiano mema yaliyopo kati ya Tanzania na Holy See ikiwemo jukumu muhimu ambalo Kanisa katoliki linafanya nchini katika nyanja za elimu na afya.
#BIMKUBWAVATICAN