DAR YATAJWA,MAENEO 10 BORA YA BIASHARA AFRIKA
HANNOVER, GERMANY
Jiji la Dar es salaam limetajwa kuwa miongoni mwa majiji bora 10 barani Afrika yanayofaa kutembelewa kibiashara kwa mwaka 2024 ambayo yanavutia mashirika ya kimataifa na wajasiriamali kutoka kote ulimwenguni.
kutokana na ripoti ya tovuti ya Givetastic kuhusu Business in Focus: (The World’s Most Popular Business Trip Destinations) jukwaa la mtandaoni la kukusanya pesa kwa ajili ya zawadi za kikundi, ambalo pia hufuatilia maeneo maarufu zaidi ya safari za biashara duniani, imezitaja Nchi za Tanzania (Dar es salaam) Nigeria (Lagos) Morocco (Marrakesh) Afrika Kusinia(Cape Town) Kenya (Nairobi) Misri (Cairo) Kenya (Mombasa) Morocco (Casablanca) Nigeria (Abuja) na Afrika kusini (Johannesburg)kuwa maeneo born kibiashara kwa mwaka huu.
Njia zilizotumika kupata takwimu hizo zimepatika baada ya Givetastic kuandaa machapisho kwenye instagram yaliyowekewa alama ya #businesstrip na kuruhusu wadau kupiga kura zao kwa kutumia hashtag (#) ambapo utafiti umejumuisha data ya baada ya janga la Covid -19 kuanzia Oktoba 2022 hadi Februari 2024.