RAIS WA POLAND ANDRZEJ DUDA KUFANYA ZIARA NCHINI FEBRUARI 8 NA 9 ,2024
Rais wa Jamhuri ya Poland Mheshimiwa Andrzej Duda anatarajia kuwa na ziara ya kikazi nchini kuanzia tarehe 8 na 9, Februari, 2024.
Mhe Duda akiwa nchini atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi.
Aidha Ziara hii ni katika hatua ya kuimarisha diplomasia ya Tanzania na Poland ambazo zina uhusiano mzuri katika miradi ya maendeleo ya miundombinu, uhifadhi wa wanyama pori, elimu, maji na usimamizi wa mazingira, utalii, biashara na uwekezaji bila kusahau ushirikiano wa mabunge.
