SHERIA YA UWEKEZAJI YA MWAKA 2022 YALETA MATOKEO CHANYA TIC
DODOMA
Taarifa kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) katika ripoti yake ya mwezi Oktoba hadi Disemba 2023 inasema imefanikisha jumla ya miradi 23 ya upanuzi yenye thamani ya shilingi 575,140,472,500 ambayo inatarajiwa kutoa ajira 5,272 huku sheria ya mpya ya uwekezaji ya mwaka 2022 ikichochea ukuaji huu katika sekta ya uwekezaji nchini.
Katika miradi hiyo ya upanuzi wawekezaji wa ndani ni 61%, wa kigeni 22%, na wawekezaji kwa njia ya Ubia ni 17%
MACHACHE KUHUSU SHERIA MPYA YA UWEKEZAJI YA MWAKA 2022.
- Sheria ya Uwekezaji Tanzania Namba 10 ya Mwaka 2022 IMETUNGWA na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 1 Novemba, 2022 na kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan tarehe 27 Novemba, 2022.
- Ni Sheria ya kuweka masharti ya uwekezaji Tanzania, kuweka masharti ya mazingira bora kwa wawekezaji, kuweka mfumo wa kitaasisi kwa ajili ya uratibu, ulinzi, uvutiaji, uhamasishaji na uwezeshaji wa uwekezaji nchini, kufuta Sheria ya Uwekezaji Tanzania, 1997 na masuala yanayohusiana na hayo.
- Sheria namba 10 ya uwekezaji mwaka 2022 imepunguza kuwa na kiwango cha mradi kutoka dola 100,000 hadi dola elfu 50.
- Pamoja na kupunguza kiwango cha uwekezaji kwa 50% bado imetoa nafasi kwa mwekezaji kupanua mradi wake ambapo hapo awali kabla ya sheria hii hakuruhusiwa.
KUMBUKA:- IMANI ya wawekezaji kwa Tanzania imeongezeka,ambapo mwaka 2023 jumla ya miradi 55 kati ya 504 iliyosajiliwa na kituo cha uwekezaji, (TIC) ilikuwa ya upanuzi wa uwekezaji uliopo tayari, huku makusanyo ya kodi yakiongezeka kwa 8% hadi shilingi trilioni 22.6 ikilingnishwa na mwaka 2022.
