RAIS SAMIA KWENYE MAZISHI YA HAYATI HAGE GEINGOB

 

RAIS SAMIA KWENYE MAZISHI YA HAYATI HAGE GEINGOB

RAIS SAMIA KWENYE MAZISHI YA HAYATI HAGE GEINGOB 

NAMIBIA 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 24 Februari, 2024 amewasili kwenye uwanja wa Michezo wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria  shughuli za mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tatu wa Namibia Marehemu Dkt. Hage Geingob Jijini Windhoek nchini Namibia.
KUMBUKA:- Februari 4, 2024  serikali ya Namibia ilitoa taarifa kuhusu kifo cha Hayati Hage Geingob, kufuatia taarifa hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kupitia mitandao ya kijamii kwa niaba ya Watanzania alitoa salaam za Pole kwa Namibia na (jana) Februari 23 Dkt Samia amewasili nchini Namibia kwa ajili ya kushiriki shughuli ya mazishi ya Mkuu huyo wa nchi Mstaafu.
BimkubwaTanzania tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kuwapa faraja wananchi wa Namibia katika kipindi hiki kigumu.