KUFUATIA VIFO VYA WATU 15 ARUSHA , DKT SAMIA ATOA POLE, AAGIZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA
NAMIBIA
Kufuatia taarifa ya vifo 15 vilivyosababishwa na magari manne kugongana eneo la Ngaramtoni Mkoani Arusha, Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa ndugu,jamaa waliopatwa na kadhia ya kuondokewa na wapendwa wao, lakini pia ametoa maagizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama na udhibiti nchini kuendea kusimamia sheria kikamilifu.
Kupitia kurasa za Twitter na Instagram za Mhe Rais Dkt Samia ameandika
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya watu 15 katika ajali iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, mkoani Arusha.
Natuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waliopoteza jamaa zao katika katika ajali hii. Ajali hizi zinachukuwa wapendwa wetu, nguvu kazi ya Taifa na mihimili ya familia. Naendelea kutoa wito kwa kila mmoja kuzingatia sheria za usalama barabarani katika matumizi ya vyombo vya moto.
Naagiza vyombo vyetu vya ulinzi, usalama na udhibiti kuendelea kuhakikisha vinasimamia sheria kikamilifu, ikiwemo ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya usafiri na udhibiti wa leseni kwa madereva wanaorudia kuvunja sheria mara nyingi na wakati mwingine kusababisha watu kupoteza maisha.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina"
Kutokana na taarifa hizi zenye kuumiza mioyo ya ndugu zetu, Bimkubwatanzania tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kuomboleza vifo vya wapendwa wetu.
POLENI SANA NGARAMTONI ARUSHA, HILI NALO LITAPITA.