BIL 3 ZAJENGA SHULE MPYA YA WASICHANA KILIMANJARO
KILIMANJARO
Serikali kwa kuhakikisha inaboresha miundo mbinu ya elimu nchini imeidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana (The Kilimanjaro Girls Secondary School) katika wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.
Shule hiyo imeanza kupokea wanafunzi Januari 2024 baada ya kukamilika kwa majengo ya vyumba na madarasa na kwa sasa ujenzi wa majengo ya utawala(ghorofa) na bwalo bado unaendelea ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wanatarajia kujiunga na kidato cha tano mwezi Mei mwaka huu.