MBAAZI YA TANZANIA KUUZWA INDIA

 

MBAAZI YA TANZANIA KUUZWA INDIA

MBAAZI YA TANZANIA KUUZWA INDIA

INDIA
Tanzania itaanza kuuza nje mbaazi katika soko la India mara moja, kutokana na uhusiano wa pande mbili uliopo kati ya nchi hizo mbili,hii ni kwa mujibu wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikisiku ya jumamosi Februari 24, kupitia ukurasa wa X (zamani wa Twitter), na kusema kuwa nchi itasafirisha mazao hayo mara moja hadi Machi 2025.
Kulingana na wizara hiyo taarifa imesema mkataba mpya utatiwa saini baada ya kumalizika kwa mkataba wa sasa kati ya Tanzania na India.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya majadiliano kati ya wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania na  Waziri wa Masuala ya Biashara wa India, Piyush Goyal, huko New Delhi, India.
Aidha, wizara imebainisha kuwa Tume ya Pamoja ya Biashara (JTC) itafanyika mwezi Aprili mwaka huu ili kuweka mikakati ya kukuza biashara kati ya Tanzania na India.