MKINGA WAMEPOKEA TSH MIL. 400 ZA KUNUNUA VIFAA TIBA
TANGA
Hadi kufikia Februari 2024 tayari kiasi cha Sh Milioni 400 zimepelekwa katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya Hospitali ya Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati ambapo taratibu za manunuzi zinaendelea.
Aidha katika mwaka wa fedha 2022/23 serikali ilipeleka kiasi cha Sh Milioni 300 za ununuzi wa vifaa tiba vinavyohitajika kwa ajili ya kuanza kutoa huduma katika vituo vya afya na zahanati zilizokamilika.
Ununuzi wa vifaa hivyo umefanikisha kuanza kutolewa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya na Zahanati 11 zilizokamilika.