MASHIRIKA YA UMMA YATAKIWA KUJIENDESHA KWA FAIDA
DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameyataka mashirika ya umma kujiendesha kwa faida ili kuepusha hasara kwa serikali.
Wito huo ameutoa leo Februari 2, 2024 akiwa anazungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini mikataba ya mauziano na uendeshaji wa kitalu cha Mnazi Bay baina ya TPDC na Kampuni ya MAUREL & PROM katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Dkt amesema “Mashirika ya umma yanatakiwa kujiendesha kisasa na kwa faida, watendaji wake wanatakiwa kufanya kazi huku wakitanguliza maslahi ya Taifa mbele”
Aidha tangu shughuli za utafutaji wa gesi asilia hapa nchini jumla ya visima 96 vimechimbwa, gesi asilia iliyogundulika inakaribia kufika futi za ujazo trilioni 57.54 ambazo futi za ujazo trilioni 10.41 zipo nchikavu na trilioni 47 zipo baharini.