SONGOSONGO & MNAZIBAY ZINAZALISHA FUTI ZA UJAZO MIL 245 ZA GESI ASILIA
DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema vitalu vya Songosongo na Mnazibay kwa pamoja vinazalisha futi za ujazo milioni 245 kwa siku huku mahitaji halisi ya gesi asilia kwa sasa ni futi za ujazo milioni 297
Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya mauziano na uendeshaji wa kitalu cha Mnazi Bay baina ya TPDC na Kampuni ya M&P katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Dkt Samia amesema Kiasi hicho kinachozalishwa kwa sasa kimechangia kuongezeka kwa umeme nchini ambapo kwa wastani umeme unaozalishwa kupitia gesi asilia ni 65% hadi 70% ya umeme wote unaozalishwa nchini.
Aidha viwanda vipatavyo 56 vimeunganishwa na matumizi ya gesi asilia hapa nchini na viwanda vingine vimeomba na vinasubiri kuunganishwa.
ZINGATIA:- Katika kufanya uendelezaji kwenye sekta ya gesi asilia serikali inashirikiana kwa ukaribu na sekta binafsi kupitia mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato,ambao unaeleza haki na wajibu wa kila m’bia kwenye makubaliano ya uzalishaji ikiwemo umiliki,mgawanyo na faida.