M-MAMA YAWALETA WA-NIGERIA NCHINI KUJIFUNZA KUPUNGUZA VIFO VYA UZAZI

 

M-MAMA YAWALETA WA-NIGERIA NCHINI KUJIFUNZA KUPUNGUZA VIFO VYA UZAZI

M-MAMA YAWALETA WA-NIGERIA NCHINI KUJIFUNZA KUPUNGUZA VIFO VYA UZAZI

DODOMA

Mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kupitia sekta ya afya katika kukabiliana na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, mama na mtoto (M-Mama) kumepelekea baadhi ya mataifa mengine ya Afrika kuja kujifunza nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu tarehe 22 Februari, 2024 Jijini Dodoma wakati wa kikao na wajumbe kutoka Serikali ya Nigeria uliongoozwa na Kamishina wa Afya wa jimbo la Borno Prof. Baba Gana, waliokuja kwa lengo la kujifunza njia za kupunguza vifo vya uzazi na mtoto kupitia mfumo wa M-mama.
Dkt. Jingu amesema mafanikio haya ambayo Serikali imeyapata ni kutokana na jitihada na bunifu mbalimbali katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto, na matokeo yameonekana na kufanya Tanzania kuwa sehemu iliyovutia mataifa mengine kuja kujifunza.
“Takwimu zinaonesha hapo awali vifo vya watoto wachanga vilikuwa 556 kati ya vizazi hai laki 100,000 na sasa idadi imepungua na kufikia  vifo 104 kwa vizazi hali laki 100,000 
Pamoja na matokeo haya chaja bado serikali ya awamu ya sita imeweka mkakati wa kuzuia vifo vinavyotokana na uzazi mama na mtoto mchanga na kwamba havikubaliki kwa sababu njia za kuvizuia zipo na zinatekelezeka kwa kuwa na jitihada na ubunifu wa uzazi salama ambao unashirikisha jamii.