UJENZI DARAJA LA JANGWANI MBIONI KUANZA

 

UJENZI DARAJA LA JANGWANI MBIONI KUANZA

UJENZI DARAJA LA JANGWANI MBIONI KUANZA

DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya  Ujenzi imeeleza kwamba ipo katika hatua za mwisho za kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Daraja katika eneo la Jangwani jijini Dar es salaam ambapo mkataba unatarajiwa kusainiwa mwezi huu Septemba 2024. (Hii ni kwa mujibu wa wizara ya ujenzi Septemba 02, jijini Dodoma).
“Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) imepanga kujenga Daraja katika eneo la Jangwani lenye urefu wa mita 390 na kimo cha mita 15 ambapo hivi sasa taratibu za manunuzi zipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wake”, imeeleza taarifa ya wizara 
Ujenzi wa Daraja la Jangwani utatumia fedha za mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa muendelezo wa Bonde la Mto Msimbazi