SGR SASA RASMI KUTOA HUDUMA JULAI 2024
DAR ES SALAAM
Treni ya umeme ya kisasa (SGR) inatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi mwezi Julai 2024 hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye kurasa za Mitandao ya kijamii za (Instagram & ( X )zamani Twitter) za Ikulu Mawasiliano.
Taarifa hiyo imekuja mara baada ya Februari 25 kufanyika zoezi la majaribio ya kawaida ya treni hiyo ya kisasa chini ya Shirika la reli Tanzania (TRC) kutoka Dar es salaam hadi Pwani huku ikitarajiwa kuendelea hadi Mkoa wa Morogoro siku za hivi karibuni.