TANZANIA KUSHIRIKI AFRICAN MINING INDABA 2024
DAR ES SALAAM
Tanzania inajiandaa kushiriki onesho la madini linalofanyika Cape Town, Afrika Kusini, (Mkutano wa African Mining Indaba 2024) kuanzia tarehe 5 hadi 8 Februari 2024.
Hatua ya Tanzania kushiriki Mkutano huo ni kampeni ya kuvutia wawekezaji kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya madini nchini.
Kupitia Mkutano huo Tanzania itashiriki katika mazungumzo na makampuni ya kimataifa yanayotoa huduma katika sekta ya madini ili kuingia ubia na makampuni ya ndani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki katika hafla hiyo kama nchi yenye sauti ya pamoja na sio ya mtu mmoja mmoja, kama ilivyofanyika kwa miaka mingi iliyopita.