MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAWANUFAISHA WANANCHI 383,293

 

MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAWANUFAISHA  WANANCHI 383,293


MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAWANUFAISHA  WANANCHI 383,293 

DODOMA
Kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria (Mama Samia Legal Aid Campaign) imewanufaisha wananchi wapatao 383,293 kutoka katika  mikoa sita nchini ya Dodoma, Manyara, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu.
Kupitia kampeni hiyo migogoro takribani 511 imetatuliwa, pia kampeni hii imeisaidia serikali/mahakama kubaini maeneo yenye migogoro mingi zaidi kwenye jamii ambayo ni maeneo ya ardhi, matunzo ya watoto,ndoa, mirathi, ukatili wa kijinsia na madai.
ZINGATIA:- Mhe. Rais  Dkt Samia amedhamiria  kuhakikisha kwamba kila Mwananchi anakuwa na ufahamu wa masuala ya Sheria ikiwemo Haki na Wajibu wake na kwamba kila Mwananchi anaifikia haki na kwa wale wasiokuwa na uwezo wa kumudu Gharama za Watoa huduma za Kisheria(Mawakili) waweze kufikiwa kupitia huduma za msaada wa Kisheria.