DKT SAMIA AUNGANA NA MABALOZI KWENYE MWAKA MPYA WAO.
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameungana na kuzungumza na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party),hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2024.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mhe Rais Samia amesema serikali itaendeleza ushirikiano na balozi hizo kwa mujibu wa katiba, tunu za kitaifa,usawa, umoja na mshikamano wa kitaifa huku akiwataka mabalozi hao kutokuingilia uchaguzi na kuzingatia mila, kanuni na maadili ya kidiplomasia.
Aidha Dkt Samia ametoa msisitizo kuhusu namna serikali ilivyojipanga kuhakikisha uchaguzi wa seriakali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu unakuwa wa haki, demekorasia, sheria na utawala bora.
