ZIARA YA RAIS WA POLAND NCHINI ANDRZEJ DUDA TAREHE 8 NA 9 FEBRUARI 2024.
Ziara hii ni ya kwanza kwa ngazi ya Rais kutoka Poland kuja nchini.
Ziara hii inalenga kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kupitia sekta za ulinzi na usalama,nishati, madini,ulinzi wa mitandao,utamaduni na uchumi wa buluu.
Atawasili nchini Februari 8(leo) na atapokelewa na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Tarehe 9 atapokelewa rasmi Ikulu, Dar es salaam na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,watafanya mazungumzo ya faragha, mazungumzo rasmi yatakayohusisha wajumbe wa pande zote mbili, na kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea waliyokubaliana katika mazungumzo yao.
Tanzania na Poland zimekuwa zikishirikiana takriban miaka 62 hadi sasa kwenye masuala ya kifedha hususan kodi,viwanda na biashara,tiba za mifugo, afya na maji
#KARIBUTANZANIAMHEANDRZEJ DUDA
