BARABARA MBEYA– CHUNYA – MAKONGOLOSI (KM 111) IMEKAMILIKA
MBEYA
Serikali imekamilisha ujenzi wa barabara km 111 kipande cha Mbeya – Chunya – Makongolosi , ambapo urefu wa km 503.36 kipande kutoka Mbeya- Rungwa – Mkiwa (km 503.36) ikiendelea kujenga kwa awamu .
Aidha Ujenzi wa sehemu ya Noranga – Itigi – Mkiwa (km 56.9) sehemu ya Noranga – Itigi (Mlongaji) (km 25.) umefikia asilimia 72 na kwa sehemu ya Noranga – Doroto (km 6) na Itigi – Mkiwa (km 25.6) kazi ya ujenzi zimeanza na utekelezaji wa mradi unaendelea.
